Kata ya Kaloleni ni mojawapo ya Kata 21 za Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ambayo ina mitaa miwili: Kaloleni na Kalimani. Ni kata ya pembezoni ambayo bado ni changa lakini iliyo na changamoto nyingi ambazo ni vyema kila mtu azitambue. Ukiipitia blog hii utaona mengi yanayofanyika na kutokea katika Kata hii hasa miradi na kazi mbalimbali za kiserikali zinazoendelea Kaloleni. Usiondoke bila kuweka maoni chini ya habari uliyosoma.
Tuesday, October 30, 2012
UJENZI WA LANGO (GETI) KUU LA SHULE SHULE YA MSINGI KALOLENI
Shule ya Msingi Kaloleni kupitia ushirikiano na Chrysalis School ilianza ujenzi wa uzio wa shule kwa kujenga fensi mwaka 2009. Kazi iliyobakia ni kuweka geti na ujio wa wageni hao umewezesha shule kuwa na geti sasa. Kwa sasa wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri kama inavyoonekana hapa:
JIKO LA SHULE LABORESHWA
Kupitia juhudi za kimashirikiano kati ya Shule hizi mbili, jiko la shule limeboreshwa. Kwa sasa Mpishi wa shule anapikia katika mazingira mazuri; jengo limeboreshwa, mfumo wa maji umeingizwa jikoni na jiko limeboreshwa kabisa.
Ujenzi ulianza mwezi wa Juni na umekamilika mwezi wa October. Ona jinsi ambavyo kazi hizi zimefanyika:
Ujenzi ulianza mwezi wa Juni na umekamilika mwezi wa October. Ona jinsi ambavyo kazi hizi zimefanyika:
SHULE YA MSINGI KALOLENI YABORESHA OFISI NA JIKO
Shule ya Msingi Kaloleni kwa mwaka huu wa 2012 imeweza kuboresha Ofisi ya waalimu, Ofisi ya Mwalimu Mkuu pamoja na kulifanyia matengenezo jiko la shule. Hii imewezekana kupitia ushirikiano ulioanza miaka mitatu iliyopita kati ya shule hii na shule moja katika jimbo la Montana huko Marekani. Wageni hawa walifika Kaloleni mwezi wa Juni na kushirikiana na wanakaloleni kufanya yote haya.
Friday, October 15, 2010
NAIBU KATIBU MKUU ALIPOTEMBELEA WAKULIMA MPUNGA KALOLENI
Naibu Katibu Mkuu - Tamisemi akiwa pamoja na Maafisa Kilimo, wahandisi pamoja na wakulima akisisitiza jambo katika chanzo cha mfereji wa Njoro ya Liwali.
MRADI WA KUJENGA TANKI LA KUHIFADHI MAJI SHULE YA MSING KALOLENI WAANZA
UJENZI WA UZIO SHULE YA MSINGI KALOLENI KARIBU KUKAMILIKA
Saturday, May 15, 2010
Subscribe to:
Comments (Atom)