Thursday, March 5, 2009

RC BABU WA KILIMANJARO AITEMBELEA KATA YA KALOLENI


Hapa Mh. Babu akielezwa maendeleo ya ujenzi na Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi , bw Gasper Mkuji huku Mkuu wa Shule akiangalia.

Mkuu wa shule akitoa maelezo kwa wageni waheshimiwa

RC. Babu akitoa hotuba fupi juu ya ziara yake Shuleni Msasani Secondari.
Aliyekaa kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa Bernadete Kinabo.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro alitembelea Kata ya Kaloleni mapema wiki hii ambapo alikuja kukagua miradi ya Maendeleo hasa shule ya sekondari Msasani na Mradi wa ujenzi wa Mfereji wa Njoro ya Goa.
Katika ziara hiyo, aliongozana na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mh. Musa Samizi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Bernadette Kinabo pamoja na wakuu wa idara mbalimbali za Manispaa na maafisa kadhaa kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.