Sunday, December 28, 2008

MATUKIO YA NYUMA KALOLENI

Chemichemi ya Goa inayohudumia wakulima lukuki inavyooneka mwezi wa Novemba. Panahitajika usafi hapa

Watoto wanaogolea kujiburudisha eneo la chemichemi ya Goa
Kuna uchafu umejikusanya ndani ya chemichemi ya Goa. Patasafishwa hivi karibuni


Diwani wa Kata ya kaloleni mwenye t-shirt nyeupe akizungumza na wakulima wa mpunga wa Kaloleni juu ya maendeleo yao.




Wakulima wa Kaloleni wakimsikiliza diwani wao alipofanya nao mkutano wa hadhara kubadilishana mawazo mwezi wa October.




Wednesday, December 24, 2008

UJENZI WA ZAHANATI UNAVYOENDELEA


Fundi akiwajibika

Mratibu wa TASAF Moshi Manispaa akiwa eneo la ujenzi kuratibu kazi pamoja na mhandisi na mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi mwenye shati la light bluu.

Mafundi mzigoni

Mhandisi wa Tasaf akielekeza mafundi pamoja na wanakamati ya ujenzi ukorogaji mzuri wa zege

Mhandisi akimgombeza mmoja wa mafundi kwa kutozingatia maelekezo

MAMBO YALIVYOKUWA MARIALE CUP


Wageni wakiongozwa na Aggrey Mariale wakienda jukwaani baada ya ukaguzi wa timu.

Bibie wachezaji wa Kilimanjaro Queens wakifurahia ushindi wa Netiboli

Kapteni wa Kaloleni United akikabidhiwa kikombe

Tuesday, December 9, 2008

KALOLENI YASHINDA FAINALI TAMASHA LA MANGI MARIALE

Kilimanjaro Qeens wakipata Kikombe na Mbuzi
Siku ya Ufunguzi wa michezo hiyo wanakaloleni, akina dada wa netiboli
Kikombe kwa kapteni wa Kaloleni United
Mabingwa wa mwaka huu Kaloleni United.
Timu ya Soka ya Kata ya Kaloleni, Kaloleni United imeshinda tamasha la mwaka huu la Mangi Mariale na kukabidhiwa Kikombe, jezi, mipira minne pamoja na ng'ombe dume baada ya kuishinda timu ya Langasani kwa bao moja kwa bila katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi.
Pia timu ya Kilimanjaro Queens ilishinda upande wa netiball kwa kupata Kikombe na Mbuzi.

Wednesday, December 3, 2008

UJENZI WA ZAHANATI UNAENDELEA VIZURI SANA

Hapa jengo la zahanati ya Kata kupitia TASAF linapandishwa kuta zake.
Baada ya hatua ya msingi ujenzi wa kujenga kuta ulianza, hapa mafundi na wananchi waliojitokeza wakifanya kazi


Ujenzi unaanzia hatua ya msingi.

Msingi unaimarishwa kwa kujazwa mawe kama inavyoonekana.



Katika Kata ya Kaloleni ni miradi kwa kwenda mbele. Mradi wa ujenzi wa zahanati ndio umeshika kasi hasa. Pichani juu ni baadhi ya hatua za mradi kuanzia hatua ya msingi hadi hivi saa. Inategemewa mapema mwakani watu wataannza kutibiwa hapa.