Monday, May 25, 2009

MKUTANO WA ULINZI MSASANI ULIVYOKUWA

Wananchi wakifuatilia majadiliano ya kikao
Mjumbe Bw. Temba akiteta jambo na wananchi wenzake kidemokrasia


Mwananchi akiomba nafasi ya kuchangia


Akina mama nao walikuwepo; hapa wakiwa makini wakifuatilia yanayosemwa.



Kata ya Kaloleni iko katika hatua za awali za kuimarisha ulinzi wa sungusungu katika mitaa yake ya Kalimani na Kaloleni. Pia wananchi wa eneo la Msasani katika Mtaa wa Kaloleni wameamua kuanzisha juhudi hizo kwa kupanga mikakati ya kuanzisha doria ya sungusungu. Katika kikao chao na uongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Kata, wananchi hao waliwapigia kura watu wanaowatuhumu kuwa ni waizi na wahalifu wa aina mbalimbali kama picha zinavyojionesha hapo juu.









KITONGOJI CHA MSASANI CHAFANYA KIKAO CHA ULINZI

Wananchi wakiwasikiliza viongozi
Mjumbe akichangia hoja ya kudumisha ulinzi


Baadhi ya vijana watakaofanya shughuli za ulinzi "sungusungu" wakiwa wametoka mbele

Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Kaloleni akiwahutubia wananchi. Waliokaa ni wenyeviti wa Mitaa na Afisa Mtendaji wa Kata. Hii ilikuwa katika kikao cha Kamati ya Ulinzi kilichofanyika tarehe 17/5/2009 kwa Mzee Tondi kuzungumzia kuibuka kwa matukio ya wizi katika eneo la Msasani.