Sunday, November 30, 2008

UJENZI WA MFEREJI WAANZA


Kupitia mpango wa maendeleo ya kilimo ya wilaya (DADP) Halmashauri ya Manispaa ya Moshi inajenga mfereji wa umwagiliaji katika eneo la Goa kwa ajili ya wakulima wa Mpunga wa Kaloleni.

Tuesday, November 25, 2008

MIRADI INAYOFANYIKA KATA YA KALOLENI KWA SASA







Kuna miradi kadhaa inayoendelezwa katika Kata ya Kaloleni kwa sasa. Panajengwa mfereji wenye urefu wa meta 1470 katika Kitivo cha kilimo cha mpunga eneo la chemichemi ya Goa.

Friday, November 21, 2008

Kwenye kata ya Kaloleni kwa sasa kuna mambo mengi tu ya kimaendeleo ambayo yanaendelea. Kwa mfano, kuna ujenzi wa miradi kama elimu, kilimo na afya.

Kuna ujenzi wa mfereji wa umwagiliaji, ujenzi wa madarasa shule ya sekondari Msasani, Ujenzi wa uzio wa shule ya Msingi Kaloleni na ujenzi wa Zahanati ya Kata.

Unaweza ukajionea mapicha kuthibitisha haya: