Friday, October 15, 2010

NAIBU KATIBU MKUU ALIPOTEMBELEA WAKULIMA MPUNGA KALOLENI

Naibu Katibu Mkuu - Tamisemi alipotembelea ujenzi wa mifereji ya umwagiliaji Kaloleni

Naibu Katibu Mkuu - Tamisemi akiwa pamoja na Maafisa Kilimo, wahandisi pamoja na wakulima akisisitiza jambo katika chanzo cha mfereji wa Njoro ya Liwali.
Mkaguzi wa Ndani Manispaa ya Moshi alipotembelea mradi wa ujenzi wa mifereji kwa ukaguzi pamona na maafisa Kilimo akihoji mambo mkulima mmoja ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Usimamizi wa Mifereji wakati wa ujenzi wa mfereji Njoro ya Liwali katika Msitu wa Njoro.



MRADI WA KUJENGA TANKI LA KUHIFADHI MAJI SHULE YA MSING KALOLENI WAANZA

Ujenzi wa Kisima tanki la maji kusaidia uhifadhi wa maji safi kwa shule
Fundi akiwajibika kujenga mahali ambapo tanki la maji safi litawekwa na kuondokana na tatizo la uhifadhi wa maji usio na tija kama wanavyoonekana wanafunzi wakichota maji kwenye kisima kilichopo shuleni ambacho hakina uwezo kuhifadhi maji mengi na kwa usalama.


UJENZI WA UZIO SHULE YA MSINGI KALOLENI KARIBU KUKAMILIKA

Ujenzi wa uzio kaloleni shule ya Msingi umefikia karibu kukamilika. Wiki hii 98% shule imezungushiwa uzio. Haya ni mafanikio ya kipindi kifupi tu cha mwaka mmoja uliopita. Pichani juu, uzio ukiwa umekutanika na uzio wa Shule ya sekondari Msasani.
Angalia uzio wa shule ya msingi Kaloleni eneo jirani na shule ya sekondari Msasani.