Sasa shule ya msingi kaloleni angalau ina mahali pazuri kwa kuandalia maakuli ya wanafunzi. Hili ndilo jiko lenyewe:
Kata ya Kaloleni ni mojawapo ya Kata 21 za Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ambayo ina mitaa miwili: Kaloleni na Kalimani. Ni kata ya pembezoni ambayo bado ni changa lakini iliyo na changamoto nyingi ambazo ni vyema kila mtu azitambue. Ukiipitia blog hii utaona mengi yanayofanyika na kutokea katika Kata hii hasa miradi na kazi mbalimbali za kiserikali zinazoendelea Kaloleni. Usiondoke bila kuweka maoni chini ya habari uliyosoma.
Tuesday, October 30, 2012
WAGENI WAONDOKA BAADA YA KAZI KUBWA KALOLENI SHULE YA MSINGI
Baada ya kushirikiana na wenyeji wao, wageni waliofika shule ya Msingi Kaloleni waliondoka kwa kuagwa rasmi kwa tafrija fupi shuleni:
WAGENI WATEMBELEA WAKAZI MITAA YA KALOLENI
Ikizingatiwa kuwa urafiki kati ya Shule ya Msingi Kaloleni na Chrysalis School ya Marekani ni wa muda mrefu sasa, wageni walijisikia kutembea na kujionea wenyewe ni jinsi gani wananchi na wakazi wa Kaloleni wanavyoishi. Walitaka kujua je wanafunzi wanaosoma shule wanayoisaidia wanatoka katika makazi na maisha ya aina gani? Walipofika mtaani waliweza kujichanganya na kushiriki katika kazi walizokuta wenyeji wao wakizifanya:
JIKO LA SHULE ULIVOENDELEA SHULE YA MSINGI KALOLENI
Kwa juhudi za binafsi za uongozi wa Kamati ya Shule baada ya wageni kuondoka, kazi ya ujenzi wa jiko imeendelea na kwa sasa imefikia hatua za mwisho kama utakavyoona:
UJENZI WA LANGO (GETI) KUU LA SHULE SHULE YA MSINGI KALOLENI
Shule ya Msingi Kaloleni kupitia ushirikiano na Chrysalis School ilianza ujenzi wa uzio wa shule kwa kujenga fensi mwaka 2009. Kazi iliyobakia ni kuweka geti na ujio wa wageni hao umewezesha shule kuwa na geti sasa. Kwa sasa wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri kama inavyoonekana hapa:
JIKO LA SHULE LABORESHWA
Kupitia juhudi za kimashirikiano kati ya Shule hizi mbili, jiko la shule limeboreshwa. Kwa sasa Mpishi wa shule anapikia katika mazingira mazuri; jengo limeboreshwa, mfumo wa maji umeingizwa jikoni na jiko limeboreshwa kabisa.
Ujenzi ulianza mwezi wa Juni na umekamilika mwezi wa October. Ona jinsi ambavyo kazi hizi zimefanyika:
Ujenzi ulianza mwezi wa Juni na umekamilika mwezi wa October. Ona jinsi ambavyo kazi hizi zimefanyika:
SHULE YA MSINGI KALOLENI YABORESHA OFISI NA JIKO
Shule ya Msingi Kaloleni kwa mwaka huu wa 2012 imeweza kuboresha Ofisi ya waalimu, Ofisi ya Mwalimu Mkuu pamoja na kulifanyia matengenezo jiko la shule. Hii imewezekana kupitia ushirikiano ulioanza miaka mitatu iliyopita kati ya shule hii na shule moja katika jimbo la Montana huko Marekani. Wageni hawa walifika Kaloleni mwezi wa Juni na kushirikiana na wanakaloleni kufanya yote haya.
Subscribe to:
Posts (Atom)