Kata ya Kaloleni ni mojawapo ya Kata 21 za Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ambayo ina mitaa miwili: Kaloleni na Kalimani. Ni kata ya pembezoni ambayo bado ni changa lakini iliyo na changamoto nyingi ambazo ni vyema kila mtu azitambue. Ukiipitia blog hii utaona mengi yanayofanyika na kutokea katika Kata hii hasa miradi na kazi mbalimbali za kiserikali zinazoendelea Kaloleni. Usiondoke bila kuweka maoni chini ya habari uliyosoma.
Tuesday, October 30, 2012
SHULE YA MSINGI KALOLENI YABORESHA OFISI NA JIKO
Shule ya Msingi Kaloleni kwa mwaka huu wa 2012 imeweza kuboresha Ofisi ya waalimu, Ofisi ya Mwalimu Mkuu pamoja na kulifanyia matengenezo jiko la shule. Hii imewezekana kupitia ushirikiano ulioanza miaka mitatu iliyopita kati ya shule hii na shule moja katika jimbo la Montana huko Marekani. Wageni hawa walifika Kaloleni mwezi wa Juni na kushirikiana na wanakaloleni kufanya yote haya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment