Kata ya Kaloleni ni mojawapo ya Kata 21 za Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ambayo ina mitaa miwili: Kaloleni na Kalimani. Ni kata ya pembezoni ambayo bado ni changa lakini iliyo na changamoto nyingi ambazo ni vyema kila mtu azitambue. Ukiipitia blog hii utaona mengi yanayofanyika na kutokea katika Kata hii hasa miradi na kazi mbalimbali za kiserikali zinazoendelea Kaloleni. Usiondoke bila kuweka maoni chini ya habari uliyosoma.
Thursday, December 17, 2009
WDC YA KUFUNGA MWAKA YAKUTANA JANA
Tuesday, December 15, 2009
Monday, December 14, 2009
Friday, October 30, 2009
Wednesday, September 16, 2009
Tuesday, September 1, 2009
DIWANI NA WENYEVITI WA MITAA WATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO KALOLENI
Saturday, August 29, 2009
AUGUST ILIVYOKUWA KALOLENI
Katika kufunga wikiendi ya mwezi wa august, Katika Kata ya Kaloleni yamefanyika mambo mengi sana. Hebu jionee mwenyewe.
Sunday, August 2, 2009
MATUKIO KALOLENI JULY
WAMAREKANI WAKIFANYA KAZI KALOLENI
Walimu wa Shule ya Msingi Kaloleni wakiwajibika pamoja na wageni
Kazi ya ukarabati ya darasa ilipokwisha, Madam Marry(Headmistress Chrysalis School, mwenye kamera akiwa na mratibu wa ziara ya wageni hao Madam Kate) wakifurahia darasa lililokarabatiwa.
Mkuu wa shule Chrysalis High School akiwa bize katika ukarabati wa darasa mojawapo.
Kazi ya ukarabati ya darasa ilipokwisha, Madam Marry(Headmistress Chrysalis School, mwenye kamera akiwa na mratibu wa ziara ya wageni hao Madam Kate) wakifurahia darasa lililokarabatiwa.
Mkuu wa shule Chrysalis High School akiwa bize katika ukarabati wa darasa mojawapo.
Walimu wakisaidiana na mmoja wa wamiliki wa Shule hiyo, Mr. Kenny katika ukarabati wa sakafu darasa la kwanza.
Kata ya Kaloleni mwezi uliopita ilipata ugeni wa kikundi cha wanafunzi na walimu wao wapatao 13 kutoka Chrysalis High School nchini Marekani. Wageni hawa waliitembelea shule ya Msingi Kaloleni na kukaa kwa siku tano wakifanya kazi za kujitolea katika kuiboresha shule hiyo.
Sunday, July 19, 2009
KALOLENI ILIPOTEMBELEWA NA WAGENI KUTOKA MAREKANI
Wanafunzi kutoka Chrysalis High School katika Jimbo la Montana wakiwa katika harakati za kubeba mchanga shughuli za ujenzi walizofanya.
Bi. Kate wa Mondo Challenge (mwenye sketi nyekundu) ambaye alikuwa mratibu wa ziara hii akiwa na wanafunzi hao muda mfupi kabla hawajaanza kukoroga zege katika kazi ya ujenzi wa uzio wa shule ya Msingi Kaloleni kama inavyoonekana.
Afisa Mtendaji wa Kata kama kiungo kikuu cha wageni hawa alijumuika nao katika kazi kila siku. Hapa pamoja na wanafunzi wawili kabla ya kazi kuanza.
Saturday, July 11, 2009
Monday, May 25, 2009
MKUTANO WA ULINZI MSASANI ULIVYOKUWA
Wananchi wakifuatilia majadiliano ya kikao
Mjumbe Bw. Temba akiteta jambo na wananchi wenzake kidemokrasia
Mwananchi akiomba nafasi ya kuchangia
Akina mama nao walikuwepo; hapa wakiwa makini wakifuatilia yanayosemwa.
Mjumbe Bw. Temba akiteta jambo na wananchi wenzake kidemokrasia
Mwananchi akiomba nafasi ya kuchangia
Akina mama nao walikuwepo; hapa wakiwa makini wakifuatilia yanayosemwa.
Kata ya Kaloleni iko katika hatua za awali za kuimarisha ulinzi wa sungusungu katika mitaa yake ya Kalimani na Kaloleni. Pia wananchi wa eneo la Msasani katika Mtaa wa Kaloleni wameamua kuanzisha juhudi hizo kwa kupanga mikakati ya kuanzisha doria ya sungusungu. Katika kikao chao na uongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Kata, wananchi hao waliwapigia kura watu wanaowatuhumu kuwa ni waizi na wahalifu wa aina mbalimbali kama picha zinavyojionesha hapo juu.
KITONGOJI CHA MSASANI CHAFANYA KIKAO CHA ULINZI
Thursday, March 5, 2009
RC BABU WA KILIMANJARO AITEMBELEA KATA YA KALOLENI
Hapa Mh. Babu akielezwa maendeleo ya ujenzi na Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi , bw Gasper Mkuji huku Mkuu wa Shule akiangalia.
RC. Babu akitoa hotuba fupi juu ya ziara yake Shuleni Msasani Secondari.
Aliyekaa kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa Bernadete Kinabo.
Katika ziara hiyo, aliongozana na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mh. Musa Samizi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Bernadette Kinabo pamoja na wakuu wa idara mbalimbali za Manispaa na maafisa kadhaa kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Subscribe to:
Posts (Atom)